Msanii wa Nako 2 Nako aacha kutumia madawa ya kulevya, ajiunga na taasisi kwa matibabu .

Unknown     10:17 PM    


Kupitia sammisago.com Rapper Ibra Da Hustler amefunguka kuwa sasa anampango wa kubadilisha maisha yake na jambo alilo anza nalo ni kuachana na matumizi ya dawa za kulevya aina ya Herion na Crack Cocaine. Da Hustler ameniambia kwenye exclusive interview niliyo mfanyia kuwa.

1] Nimeacha Kabisa madawa na nina siku nne sijagusa toka nimejiunga na hii taasisi, nimejifunza kuvumilia arosto na matumaini yangu ni kuacha kabisa madawa kwani yameharibu maisha yangu kabisa. Ni Uharibifu wa pesa nyingi na umekaribisha dharau kwenye maisha yangu

2] Nikifanikiwa kuwa sober kabisa mpango wangu ni kurudi vizuri kwenye mziki kwani ndio uwezo wa kazi nilionao na najua mashabiki bado wana hamu na kazi zangu.

3] Nako 2 Nako na Weusi wananipa ushirikiano mzuri sana, wote wamefurahi kusikia nimeacha madawa na Lord ndio aliye nipigia simu kuniambia nimefanya jambo msingi.

4] Yes ni kweli kuna binti alini shawishi kutumia madawa na ndio najutankumfahamu na kwanini nilikubali. Nimegungua hataki maendeleo yangu kabisa nanimejifunza kutoka kwake, sasa nikimuambia mtu usiguse madawa ataamini kwani najua kitu gani atapata kwenye maisha yake.

5] Wimbo Wa Sababu Ni Wewe Nimeimba mambo yote yaliyo nitokea toka nimeanza kutumia madawa na jinsi yalivyo mess up my life, Matumaini yangu vijana watajifunza kutokwa kwangu kuhusu madhara ya hii kitu.

SOURCE Sammisago.com
LIKE PAGE YETU HAPA ILI UWEZE KUPATA HABARI ZETU KUPITIA AKAUNTI YAKO YA FACEBOOK KILA SIKU.

Recommended

Like Us

Company

Legal Stuff

FAQ's

Blogroll

Subscribe to Newsletter

We'll never share your Email address.
© 2015 Umbeya Specially. Blogger Templates Designed by Bloggertheme9. Powered by Blogger.