| Dada anaetuhumiwa kukamatwa na madawa ya kulevya. |
Akizungumza na Gazeti la Mwananchi jana Mkuu wa Kitengo cha Habari cha Wizara ya Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa, Mkubwa Ali, alikiri kukamatwa kwa watu hao (majina yanahifadhiwa) ambao mmoja ni mkazi wa Ilala na mwingine wa Magomeni jijini Dar es Salaam. “Taarifa tulizonazo zilizo rasmi kutoka Ubalozi wa Tanzania nchini Misri kwa sasa ni kukamatwa kwa Watanzania wawili waliokuwa wakisafirisha heroin kuelekea Bara la Asia na walikamatwa nchini Misri wiki mbili zilizopita.”