Watu sita wazimia Leaders wakati wanaaga mwili wa marehemu NGWAIR

Unknown     2:29 AM    

Mmoja wa shabiki wa marehemu Albert Mangwea aliyeanguka na kupoteza fahamu wakati kuuaga mwili wa msanii huyo katika viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam.Picha na KALI ZA KITAA MAGAZINE              Editruda Mashimi,Dar es Salaam
WATU sita wameanguka na kupoteza fahamu wakati wa kuuaga mwili wa aliyekuwa msanii wa muziki wa Kizazi kipya nchini Tanzania katika viwanja vya Leaders Club, watu hao ni wanawake wanne na wanaume wawili na wanaendelea kupewa huduma ya kwanza kutoka kwa kikosi cha msalaba mwekundu waliopo katika viwanja hivi na kuwapa huduma ya kwanza.
Mwandishi wa Kali za kitaa magazine akiwa katika viwanja hivyo jijini Dar es Salaam anasema kwamba umati mkubwa umezidi kuongezeka katika viwanja hivyo huku vilio vikitawala.
Wasanii wa muziki wa Kizazi Kipya wakiongozwa na msanii maarufu Abdul Nassib (Diamond Platinumz) wamejitokeza kwa wingi katika tukio hilo kihistoria katika tasnia ya muziki wa kizazi kipya.
Akizungumza  katika viwanja hivyo msanii aliyewahi kutamba na kibao chake cha kwanza cha Zeze langu T.I.D ambaye kwa sasa anatamba na Bendi yake ya muziki ya Top Band amesema kwamba, "Kuna mipango mingi tulipanga na Mangwea lakini leo nasikitika sana kuona nimebaki peke yangu".
LIKE PAGE YETU HAPA ILI UWEZE KUPATA HABARI ZETU KUPITIA AKAUNTI YAKO YA FACEBOOK KILA SIKU.

,

Recommended

Like Us

Company

Legal Stuff

FAQ's

Blogroll

Subscribe to Newsletter

We'll never share your Email address.
© 2015 Umbeya Specially. Blogger Templates Designed by Bloggertheme9. Powered by Blogger.