Vanessa Mdee aumbuliwa na kivazi chake kwenye tuzo kilimanjaro....!!!!

Unknown     6:00 PM    


 MSANII wa muziki wa kizazi kipya Vanessa Mdee kivazi chamuumbua katika tuzo za Tanzania Kilimanjaro Music Awards zilizofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita jijini Dar es Salaam.

Msanii huyo alijikuta akishindwa kutembea huku akijiziba mbele kutokana na kigauni alichokuwa amevaa kuwa na mipasuo huku kukiacha sehemu kubwa ya mwili wake.


Vanessa alionekana kuwa na wasiwasi kila alipopanda jukwaani huku akiziba mipasuo ya nguo yake ili kuepusha aibu ya kuonyesha mapaja yake kutokana na mipasuo ya kivazi hicho.

Baadhi ya watazamaji waliofika ukumbini hapo walionekana kushangazwa na kitendo hiko huku wengine wakiohoji kwa nini ameamua kuva hivyo huku akipata wasiwasi wa kuficha sehemu ya mwili wake ili usionekane.

"Kwa nini ameamua kuvaa gauni hilo wakati anajua lina mipasuo mirefu ni bora angeacha tu kuliko hivyo anavyopata shida nalo kwa kulishika kuzuia hiyo mipasuo" alisema mdau mmoja aliyehudhuria tuzo hizo.
LIKE PAGE YETU HAPA ILI UWEZE KUPATA HABARI ZETU KUPITIA AKAUNTI YAKO YA FACEBOOK KILA SIKU.

Recommended

Like Us

Company

Legal Stuff

FAQ's

Blogroll

Subscribe to Newsletter

We'll never share your Email address.
© 2015 Umbeya Specially. Blogger Templates Designed by Bloggertheme9. Powered by Blogger.