Sanduku lenye Mwili wa msanii bongofleva,Marehemu Albert Mangwea ukishushwa kaburini taratibu na waombolezaji,ndugu jamaa na marafiki jioni ya jana kwenye makaburi ya Kihonda nje kidogo ya Mji wa Morogoro,ambapo maekfu ya watu walishuhudia mazishi hayo yaliyovunja rekodi mkoani humo.
Eeneo la Mazishi likiendelea kama lionekanavyo kwa mbaali.
Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakirekodi yaliyokuwa yakijiri kwenye mazishi hayo.
Ibada ya mazishi ikiendelea kabla ya sanduku la marehemu Albert Mangwea kushushwa kaburini. Na pichani chini ni baadhi ya watu wakianza kuondoka sehemu ya mazishi.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro,Mh Joel Bendera akizungumza machache ndani ya uwanja wa Jamuhuri wakati watu mbalimbali walijitokeza kuaga mwili wa Msanii Albert Mangwea.
Pichani kulia ni Mh Joseph Mbilinyi a.k.a Sugu sambamba na ndugu jamaa na marafiki wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri uwanjani hapo wakati wa sala ya kumuombea marehemu Mangwea ikiendelea.
Msanii Mkongwe wa muziki wa kizazi kipya,Afande Sele sambambana na watu wengine wakielekea kutoa heshima zao za mwisho






















