Mwigulu naye adai kuwa bomu lilirushwa na chadema...."kama sio wao, mchukua video alitaarifiwa na nani kwamba bomu litarushwa???"

Unknown     11:52 AM    


Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Mwigulu Nchemba  amesema bungeni leo kwamba Chadema ilipanga kufanya shambulio la bomu kwenye mkutano wa Soweto jijini Arusha.

Amesema hakuna jambo ambalo Chadema wamewahi kupanga wakashindwa.

“Itakuaje mtu amechukua mkanda wa tukio la umwagaji wa damu bila kutikisika au mchukuaji kukimbia, haiwezekani- hiyo walipanga.

“Inakuaje amechukua mkanda wa video kama mkanda wa harusi, yaani kama mkanda wa sendoff.? Amehoji Mwigulu huku wabunge wa CCM wakimuunga mkono kwa kupiga meza bungeni.


Mapema wiki hii katika mkutano wa Chadema, mtu mmoja asiyefahamika alirusha bomu kwenye mkutano wa Chadema na kusababisha watu wanne  kufariki dunia na wengine 68 kujeruhiwa na kupelekwa katika Hospitali ya Mt Meru, Arusha.
LIKE PAGE YETU HAPA ILI UWEZE KUPATA HABARI ZETU KUPITIA AKAUNTI YAKO YA FACEBOOK KILA SIKU.

,

Recommended

Like Us

Company

Legal Stuff

FAQ's

Blogroll

Subscribe to Newsletter

We'll never share your Email address.
© 2015 Umbeya Specially. Blogger Templates Designed by Bloggertheme9. Powered by Blogger.