Mtangazaji wa Times fm Khadija Shaibu ajianika "akijisaidia" chooni

Unknown     7:22 AM    



MTANGAZAJI wa Kituo cha Redio cha Times FM, Khadija Shaibu ‘Dida’ amewashangaza watu baada ya kutundika mtandaoni picha zinazomuonesha akioga bafuni huku nyingine akiwa chooni  akikata  gogo.



Picha hizo zinapatikana kwenye mtandao wake na hakueleza ilikuwa wapi ila akasema ilikuwa ni siku alipoamua kuitumia wikiendi yake ipasavyo katika hoteli ambayo hakuitaja jina.
 
Baadhi ya watu waliyoziona picha hizo walimponda wakidai eti ni ulimbukeni lakini wapo waliomtetea kwa kusema, ni staili tu ya maisha aliyoamua kuishi.





“Ushamba tu, ndo nini sasa?  alisema mmoja wa wadau huku mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Dick akisema: “Msimuonee wivu mwenzenu, anakula bata zake na nyie hamjakatazwa.”
 
Dida alipoulizwa kuhusu kujianika hivyo alisema, hizo ni ishu zake binafsi na wapenzi wake wanapenda kuona kila anachokifanya, ndiyo maana anawawekea kwenye blogu yake.

BAADHI  YA  MAONI  YA  WATU  KATIKA  BLOG  YAKE 

LIKE PAGE YETU HAPA ILI UWEZE KUPATA HABARI ZETU KUPITIA AKAUNTI YAKO YA FACEBOOK KILA SIKU.

Recommended

Like Us

Company

Legal Stuff

FAQ's

Blogroll

Subscribe to Newsletter

We'll never share your Email address.
© 2015 Umbeya Specially. Blogger Templates Designed by Bloggertheme9. Powered by Blogger.