"Tutaonyesha mkanda wa mauaji ya bomu ya Arusha ili dunia ijue kuwa serikali ya CCM inamwaga damu za raia wake makusudi"....John Mnyika.

Unknown     5:42 AM    

Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa CHADEMA, John Mnyika (MB - Ubungo) amesema chama chake kitatoa mkanda wa video unaoonesha ulipuaji na shambulio lililofanyika katika viwanja vya Soweto (AICC) Arusha siku ya Jumamosi, Juni 15, 2013 wakati wa kufunga kampeni za uchaguzi wa udiwani za Kata za mkoa huo.

Mnyika amesema wataukabishi si tu kwa Polisi baada ya kupata ushauri wa kisheria, hasa baada ya Polisi kuonyesha kutokuwa na nia nzuri, bali watauweka hadharani, “kabla ya polisi kujua kuwa CHADEMA ina mkanda, polisi walishahisi kuna recording imefanyika, kwa hiyo wakaanza kutafuta watu wanaodaiwa kuwa wamerekodi na kuwakamata na kuwapiga na kuwatesa, badala ya kuwachukulia kama raia wema wa kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi. Katika mazingira haya ya jeshi la polisi, kuonekana kwamba linataka ushahidi siyo kwa njia njema, timu yetu iliyoko Arusha, ikiongozwa na Mwenyekiti, imeamua kwamba, kabla ya kutoa huo mkanda kwa umma, tukae na jopo letu la wanasheria. Mkanda huu tutautoa, wazi kabisa, ili Watanzania na Dunia ijue kwamba Serikali hii inatumia umwagaji damu kubaki madarakani, halafu inageuza kuwa CHADEMA ndiyo inayofanya hivi vitendo...”

LIKE PAGE YETU HAPA ILI UWEZE KUPATA HABARI ZETU KUPITIA AKAUNTI YAKO YA FACEBOOK KILA SIKU.

,

Recommended

Like Us

Company

Legal Stuff

FAQ's

Blogroll

Subscribe to Newsletter

We'll never share your Email address.
© 2015 Umbeya Specially. Blogger Templates Designed by Bloggertheme9. Powered by Blogger.