Maneno huumba....!!! Huddah ameliaga shindano hilo...------------------------Huddah ambaye ni mshiriki kutoka Kenya alijikuta akibubujikwa na machozi jana wakati akimuelezea Angelo (SA) kuhusiana na uhusiano wake wa kimapenzi ambao ni wa ku-beep yani vuta nikuvute ambao amekuwa nao nchini kwao. |
KWA UPANDE MWINGINE, mrembo wa Tanzania ,Feza anayeiwakilisha Tanzania alijikuta katika simanzi kali wakati alipoelezea kuhusu jinsi ambavyo kaka yake aliteseka kutokana na kujihusisha na madawa ya kulevya .. 'drugs'.Feza alitumia fursa hiyo kuwasihi watu hasa vijana kujiepusha kabisa na madawa ya kulevya kwani ni hatari sana katika jamii inayotuzunguka.. |

