Hili Tamko La FIFA La Mfurahisha Mario Balotelli.

Unknown     12:37 PM    


Mshambuliaji nyota wa klabu ya AC Milan super Mario baloteli,ameeleza kufurahishwa kwake na hatua ya shirikisho la kandanda la dunia fifa,kutangaza hatua kali za kupambana na matukio ya kibaguzi kwenye soka duniani.Balotel ambaye amewahi kukutana na matukio kadhaa ya ubaguzi na mara nyingine akifananishwa na nyani,amepongeza hatua hiyo ya fifa ya kulishughulikia suala hilo kupitia mtandao wa kijamii wa twitter.

Ikumbukwe kwamba vitendo vya Ubaguzi wa rangi ambavyo vimefanywa na mashabiki wa Klabu ya Pro Patria ya nchini Italia kwenye mchezo dhidi ya AC Milan, vilisababisha kusimamishwa na nusura kuvunjika kwa mchezo huo huku wachezaji weusi wakionekana kukasirishwa na kitendo hicho.Wachezaji wa AC Milan wakiongozwa na Kevin-Prince Boateng ambaye alivua shati na kisha kupiga mpira upande wa mashabiki waliokuwa wanafanya ubaguzi wa rangi na kisha kufuatwa na wachezaji wengine weusi.
Ndipo shirikisho la Soka Nchini Italia FIGC likametangaza kufanya uchunguzi kubaini wale ambao wamehusika kwenye kufanya vitendo hivyo vya kibaguzi,ambapo mwamuzi alisimamisha mchezo katika  dakika ya 25 baada ya Boateng kuchukizwa na maneno ya kibaguzi ambayo yalikuwa yanatolewa dhidi yake na wachezaji wengine weusi hatua iliyomfanya awapige mashabiki hao na mpira.

Wachezaji wengine weusi wa AC Milan ambao walikumbana na ubaguzi huo wa rangi kutoka kwa mashabiki wa Klabu ya Pro Patria ni pamoja na M'Baye Niang, Urby Emanuelson na Sulley Muntari. Kocha Mkuu wa AC Milan Massimiliano Allegri baada ya kuvunjika kwa mchezo huo akawaambia wanahabari wamechukizwa mno na kitendo kilichofanywa na mashabiki wa klabu ya Pro Patria. Licha ya juhudi kubwa kufanywa Barani Ulaya kuhakikisha vitendo vya ubaguzi vinamalizwa michezoni lakini kwa baadhi ya mashabiki wa mpira wa miguu wamekuwa hawaliewi hilo na badala yake wamekuwa mstari wa mbele kuendeleza vitendoi hivyo.

Hivi karibuni klabu ya Inter Milan ya Italia imeshitakiwa kwa tabia za kibaguzi za mashabiki walizozionyesha wakati wa mchezo wa Europa League dhidi ya Tottenham Hotspurs hivi karibuni.
Na shirikisho la Soka barani Ulaya-UEFA likaituhumu klabu hiyo kwa kukosa ushirikiano na kurusha vitu mbalimbali wakati wa mchezo huo. Inter tayari wameshapigwa faini ya paundi 43,000 na maofisa wa Ligi Kuu nchini Italia msimu uliopita, baada ya mashabiki wake kukutwa na hatia ya kuwafanyia vitendo vya kibaguzi wachezaji wa zamani wa klabu hiyo Mario Balotelli na Sulley Muntari.

Akizungumza katika kikao cha wajumbe wa FIFA mjini Port Louis, Mauritania, Blatter amesema kuwa ana furaha FIFA hatimaye imejinyanyua baaada ya kukabiliwa na changamoto chungu nzima kuhusu ubaguzi.FIFA imechukua hatua kuhusiana na ubaguzi wa rangi, na sasa timu zitakabiliwa na adhabu kali kwa kupatikana na hatia ya tukio baya la kibaguzi, ikiwa ni pamoja na kupokonywa pointi na kushushwa daraja.

Hatua hizo zimeidhinishwa kwa wingi na zinafuatia matatizo ya karibuni nchini Italia na England. Kulingana na sheria hizo mpya, makosa makubwa au ya kurudiwa yatakayofanywa na klabu au mashabiki wake yatasababisha pia kupigwa marufuku timu kushiriki katika vinyang'anyiro fulani ikiwa ni pamoja na ligi ya mabingwa Ulaya – Champions League.

Hata hivyo baadhi wanasisitiza kuwa FIFA haifanyi ya kutosha. Rais wa shirikisho hilo Sepp Blatter, hata hivyo ametoshelezwa na hatua hizo kufuatia kashfa zilizoshuhudiwa katika miaka kadhaa ya nyuma.
LIKE PAGE YETU HAPA ILI UWEZE KUPATA HABARI ZETU KUPITIA AKAUNTI YAKO YA FACEBOOK KILA SIKU.

,

Recommended

Like Us

Company

Legal Stuff

FAQ's

Blogroll

Subscribe to Newsletter

We'll never share your Email address.
© 2015 Umbeya Specially. Blogger Templates Designed by Bloggertheme9. Powered by Blogger.