Diamond akana kukopa fedha kwenye shirika la uchangishaji fedha za mikopo..!!

Unknown     9:26 AM    

Kumekuwa na taarifa za Diamond Platnumz kuwachangisha watu fedha kupitia facebook page yake ya DIAMOND PLATNUMZ, Diamond asema yeye hakutoa ridhaa hiyo ya watu kuchanga pesa kuhusu mikopo … So ametoa taarifa mpya ya kukataa kuhusika na michango hiyo ambayo ni hii hapa …
“TAARIFA MAALUMU KUHUSU POST YA MIKOPO ILIYOWEKWA KWENYE FACEBOOK ACCOUNT YA DIAMOND PLATNUMZ
Habari rafiki, ndugu na mashabiki zangu wote kwa ujumla, kwa wale wanaofatilia Facebook Account zangu yani diamondplatnumz mtakumbukamchana wa leo kuna post ilitumwa kupitia account zangu za facebook ikihusu mambo ya mikopo na kuwataka watu wachangie, ukweli ni kwamba hiyo post imewekwa pasipo ridhaa yangu baada ya watu ambao sawafahamu ku-hack acount yangu na kufanya kitendo hicho, mimi kama Diamond na team yangu nzima ya WASAFI tunaomba radhi kwa usumbufu wowote uliojitokeza,na 
tunaendelea kufuatilia jinsi ya kuwatia mbaroni waharifu hao wa ku hack acount na kuwafikisha sehem husika ili iwe fundisho kwa wote wenye tabia hiyo.”

Recommended

Like Us

Company

Legal Stuff

FAQ's

Blogroll

Subscribe to Newsletter

We'll never share your Email address.
© 2015 Umbeya Specially. Blogger Templates Designed by Bloggertheme9. Powered by Blogger.