Baba yake Diamond yupo hoi anaumwa......Diamond hajawahi kanyaga kumjulia hali...!!

Unknown     2:54 AM    

BABA wa msanii Nasibu Abdul ‘Diamond’, Abdul Juma yupo hoi akisumbuliwa na ugonjwa wa miguu.
 

Kwa mujibu wa chanzo makini, Baba Diamond anasumbuliwa na tatizo la miguu kuvimba hali ambayo imemfanya ashindwe kutembea lakini cha kushangaza mwanaye, Diamond hajaenda kumjulia hali.

“Baba Diamond ni mgonjwa kwa muda mrefu sana lakini Diamond hajawahi kuja kumuona hata siku moja,” kilisema chanzo hicho.

Baada ya kuzinyaka habari hizo, waandishi  wetu walifunga safari mpaka nyumbani kwa mzee huyo, Magomeni-Kagera, jijini Dar ambapo alikiri kuugua kwa muda mrefu na kukosa msaada kutoka kwa Diamond.

“Nasumbuliwa na miguu kwa muda mrefu sana na ninatibiwa katika Hospitali ya Saint Monica, Manzese-Darajani. Diamond ana taarifa za kuumwa kwangu lakini hajawahi kuja kuniona.

“Namshukuru mwanangu Queen Doreen kwa kunijali kwa kila kitu,” alisema baba Diamond.

LIKE PAGE YETU HAPA ILI UWEZE KUPATA HABARI ZETU KUPITIA AKAUNTI YAKO YA FACEBOOK KILA SIKU.

Recommended

Like Us

Company

Legal Stuff

FAQ's

Blogroll

Subscribe to Newsletter

We'll never share your Email address.
© 2015 Umbeya Specially. Blogger Templates Designed by Bloggertheme9. Powered by Blogger.