TID AWALALAMIKIA KILL MUSIC AWARDS KWA KUTOWEKA NYIMBO YAKE KTK TUZO HIZO, HIKI NDO ALICHOKISEMA

Unknown     2:06 PM    


419273_10150648783418749_340086305_n
Hatimaye Mnyama TID ameamua kuvunja ukimya na kuzungumzia suala la kukosa kutajwa kuwania tuzo za Kili mwaka huu na kudai anahisi amehujumiwa. Akiongea exclusively na Bongo5, TID amesema ameshangaa wimbo wake Kiuno kutoingizwa kwenye tuzo hizo ilhali ulifanya vizuri kwenye redio na kwenye TV.
“Waliniita before hata hizo nominations na nini, mimi nilikuwa safarini nikashindwa kufika na tayari nilishaongea na Kavishe tulikuwa gym tukakubaliana kwamba hizi issue ziishe sasa nashangaa kwenye nominations sijawekwa na wimbo wangu sijui maana yake nini,” amesema TID.
Amesema hawezi kuilaumu academy inayochagua nominations hizo kwakuwa hupelekewa majina.
“Hapo kuna kauli imetoka ya mtu mwingine ambaye amekataza nisiwekwe,” amesisitiza.
Amesema tayari alishakubali kuziweka tofauti zake na waandaji wa tuzo hizo pembeni ili kuanza ukurasa mpya lakini haelewi ni kipi alichowakosea mara nyingine.
“Kwanini sasa wasiniweke, nini kitu kibaya nilichofanya mimi? Nahisi kuna mchezo kwasababu wimbo wangu ulitakuwa uingie kwenye categories kibao na ushinde sababu umehit sana mwaka jana.”

,

Recommended

Like Us

Company

Legal Stuff

FAQ's

Blogroll

Subscribe to Newsletter

We'll never share your Email address.
© 2015 Umbeya Specially. Blogger Templates Designed by Bloggertheme9. Powered by Blogger.