Sugu amkaribisha profesa Jay Mjengoni 2015! Apewa kadi rasmi ya Chadema. Jide na kufuata kadi.

Unknown     5:36 AM    

 
Rapper mkongwe nchini, Joseph Haule aka Profesa Jay amejiunga rasmi na Chama cha Demokrasia na Maendeleo, CHADEMA. Profesa amekabidhiwa kadi ya uanachama wa CHADEMA na mbunge wa Mbeya mjini, Joseph Mbilinyi aka Sugu. Kujiunga rasmi kwa Profesa kwenye chama hicho kunaashiria kuwa huenda akawa na nia ya kugombea ubunge kwa tiketi ya chama hicho mwaka 2015
 
The heavy weight MC Proj Jay, aka Dady, Joseph Haule akipokea Kadi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kutoka kwa Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi aka Sugu Muda mfupi uliopita Mjini Dodoma Mara baada ya kujiunga rasmi na Chadema

Muda si mrefu msanii maarufu hapa Bongo Profesa Jay (Joseph Haule) amejiunga na Chama Cha Demokrasi na Maendeleo huko Dodoma na amekabidhiwa tiketi ya chama cha CHADEMA rasmi na Mbunge wa Mbeya Joseph Mbilinyi aka Sugu huko Dodoma.
Na taarifa za Chini ya Kapeti zinasema kuwa Lady Jay Dee pamoja na Mumewe Gadner G Habash nao wamejiunga na Chama Hicho Cha Chadema.Tunazidi kutafuta habari hizi za lady Jay Dee na Mumewe kujiunga na Chadema na tutataarifiana kadri tunavyozidi kuzipata

Recommended

Like Us

Company

Legal Stuff

FAQ's

Blogroll

Subscribe to Newsletter

We'll never share your Email address.
© 2015 Umbeya Specially. Blogger Templates Designed by Bloggertheme9. Powered by Blogger.