Naona huruma kumpiga chini, nifanyaje?

Unknown     11:51 PM    

Hapo kati mamsapu aliniletea sana za kuleta na siku moja akanitamkia wazi kuwa amechoka kuishi na mimi (baadae aliomba msamaha akasema alipandwa na hasira). Kipindi tulichochuniana nikakutana na kadem fulani na nikawa nimeamua mamsap akisepa tu, navuta jumla hako kadada.(ni kadada kwa sababu kiumri nakazidi sana halafu ni kipotabo). Sasa wife hakusepa wala nini na mimi nikawa nimekolea nje mpaka nimepangishia chumba na gheto nimelikamilisha. Wife alikuja futa kauli zake za kuondoka hazingui tena na kawa mpole na mwenye heshima mpaka naona aibu kuendelea na nyumba ndogo. Wife Sitaki kumwacha na nyumba ndogo naona huruma kummwaga kwa sababu yaani kakolea kishenzi. Sidhani kama atamwamini mwanaume mwingine Mimi nikimtosa. Naogopa kumwambia wife nataka oa mke wa pili kwa sababu atasepa, japo ningewamudu na napenda wake wawili. Kitu kingine mamsap hapendi kujishughulisha na utafutaji hela wakati hii nyumba ndogo inajituma kwenye utafutaji kishenzi (mchaga), mara kadhaa ashanikwamua kwenye vishida vya lakilaki hizi. Sasa nipo kwenye dilemma!!

,

Recommended

Like Us

Company

Legal Stuff

FAQ's

Blogroll

Subscribe to Newsletter

We'll never share your Email address.
© 2015 Umbeya Specially. Blogger Templates Designed by Bloggertheme9. Powered by Blogger.