Mkenya aliyejibadilisha jinsia na kuwa mwanamke aitaka wizara ya elimu kubadilisha sehemu ya jinsia kwenye vyeti vyake na kuandikwa mwanamke...!!

Unknown     5:36 AM    



Afisa Mkuu Mtendaji wa Baraza la Kitaifa la Mitihani (KNEC) Paul Wasanga.

BAADA YA KUJIBADILISHA

BAADA YA KUJIBADILISHA



MWANAUME aliyegeuza jinsia yake, amelishtaki baraza la mitihani nchini, Kenya National Examination Council (KNEC), akitaka lishurutishwe kubadilisha
vyeti vyake kuonyesha kwamba ni mwanamke.

Bi Audrey Mbugua ambaye awali alifahamika kwa jina la Andrew Ithibu kabla ya kubadilisha jinsia yake, anataka cheti chake cha mtihani wa kidato cha nne (KCSE) kionyeshe kwamba ni mwanamke.

Aliambia mahakama kwamba aligunduliwa kuwa na dosari ya jinsia 2001, na amekuwa akikabiliana na shida nyingi kwa sababu anatambuliwa kama mwanaume katika vyeti vyake.

“Nimejaribu kuomba KNEC mara nyingi ibadilishe jina langu katika cheti changu vya mtihani wa KCSE ili kionyeshe jinsia yangu halisi bila kufaulu,” Bi Audrey aliambia mahakama.

Alisema hatua ya KNEC kukataa kufanya mabadiliko hayo, imemsababishia mateso mengi kwa kubaguliwa na kunyimwa kazi. Mahakama ilimruhusu kuwasilisha ombi la kutaka baraza hilo liagizwe kutekeleza majukumu yake kwa kurekebisha jina lake liwe na mwanamke.

Siku 14

Anataka pia baraza hilo iagizwe kubadilisha alama inayoonyesha jinsia yake inayoonyesha ni mwanaume katika cheti hicho na badala yake ionyeshe kuwa ni mwanamke.

Mahakama ilipatia KNEC na Mkuu wa sheria muda wa siku 14 kujibu ombi la Bi Audrey.

Kesi itatajwa Mei 28 ili mahakama itoe maagizo zaidi.

CREDT: GUMZO LA JIJI

Recommended

Like Us

Company

Legal Stuff

FAQ's

Blogroll

Subscribe to Newsletter

We'll never share your Email address.
© 2015 Umbeya Specially. Blogger Templates Designed by Bloggertheme9. Powered by Blogger.