MAMA KANUMBA: chondechonde, kaburi la mwanangu lisigeuzwe mtaji

Unknown     10:12 AM    


BAADA ya siku za hivi karibuni kubainika kuwa baadhi ya vijana wanaolinda makaburi ya Kinondoni wamegeuza mtaji kaburi la aliyekuwa msanii maarufu wa filamu Bongo, marehemu Steven Kanumba, mama mzazi Flora Mtegoa amewaomba wahusika kuacha mchezo huo mara moja.
Akizungumza kwa huzuni mama Kanumba alisema alihuzunishwa sana na kitendo hicho cha kaburi la mwanaye kugeuzwa mtaji na kumtaka mtu yeyote atakayetozwa pesa aripoti polisi mara moja.
“Inaniuma sana na naiomba serikali na watu wengine wanisaidie jamani kwa sababu wanaofanya biashara hiyo ya kulipisha watu kwa ajili ya kuliona kaburi wanakosea,” alisema Mama Kanumba.
Hivi karibuni ilibainika kuwa baadhi ya vijana wanaotunza makaburi ya Kinondoni wanatoza shilingi 5,000 kwa watu wanaotoka mikoani kwa ajili ya kuliona kaburi la Kanumba na kupiga picha.
chanzo:globalpublishers

Recommended

Like Us

Company

Legal Stuff

FAQ's

Blogroll

Subscribe to Newsletter

We'll never share your Email address.
© 2015 Umbeya Specially. Blogger Templates Designed by Bloggertheme9. Powered by Blogger.