Dodoma. Wakati mkutano wa 11 wa Bunge ukiendelea mjini Dodoma, Mbunge wa Mwibara Kangi Lugola (CCM), ameendelea kuwa mwiba kwa Serikali yake huku akisema hakuna wa kumnyamazisha kuhusu hoja za kutetea Watanzania, kwa mambo yasiyofaa.
Katika mahojiano na Mwananchi Jumapili, mbunge huyo ameeleza ya moyoni kuwa amekuwa akipingana na hoja za Serikali ikiwamo inayohusu bajeti zake ambazo alisema nyingi zimewekwa kinadharia.
“Nashukuru kwa kutaka kujua ukweli juu yangu, mara nyingi watu wamekuwa wakinituhumu mimi na wabunge wengine kuwa tunaisaliti Serikali na chama chetu, huo ni unafiki maana wanaoisaliti ni hao wakina ‘ndiyo mzee,’’anaanza kusimulia.
Swali. Nini maana yake unaposema wanaoisaliti CCM ni hao wanaokubali kila kitu, kwani kukubali na kupinga huoni ni tofauti na kwamba anayepinga ndiye msaliti.
Jibu: Ngoja nikwambie (mwandishi), sisi tunaopinga baadhi ya bajeti za wizara ndiyo tunaojua uchungu wa chama chetu kwa sababu tunataka chama kiendelee kubaki madarakani, lakini hao wanaopitisha pamoja na madudu si wema kwa chama hata siku moja, watakosa majibu siku ya mwisho.
Akitetea hoja hiyo anaeleza kuwa, Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzim imeainisha mambo mengi yanayotakiwa kutekelezwa.
Anasema hata hivyo baadhi ya wabunge wanafanya kila kitu kwa kujipendekeza bila ya kujua kwamba kupitisha madudu hakufanyi ilani itekelezwe kwa wakati.
Anasema hata hivyo baadhi ya wabunge wanafanya kila kitu kwa kujipendekeza bila ya kujua kwamba kupitisha madudu hakufanyi ilani itekelezwe kwa wakati.
Swali. Kwani usipounga mkono ndiyo mambo yanatekelezwa.
Jibu. Ujue kuwa wakati wa uchaguzi mkuu vyama huenda kuomba ridhaa ya wananchi waviunge mkono, jambo hilo linakwenda sambasamba na ahadi zisizotekelezeka, sasa usipokuwa makini na hizo bajeti, unadhani utafanyaje mwisho wa siku kama si kuambulia patupu.

Anasema bajeti nyingi za Serikali huwa hazitoi majibu hata kidogo, lakini wabunge wamekuwa wakiogopa kuzikataa kwa kuhofia kuwa wataambiwa wanapingana na Serikali yao.
Swali. Inasemekana kwamba umewekwa katika orodha ya wabunge wasaliti wa CCM na kwamba wabunge wamepanga kuwashtaki katika vikao vya juu vya chama hicho, unazungumziaje jambo hilo.
Jibu. Taarifa hizo ni kweli, lakini kunishtaki hakutaniziba mdomo na badala yake kutaniongezea kasi ya mapambano katika haki kwa maslahi ya wapiga kura wangu na Watanzania wote.
Swali. Inaonekana katika orodha yenu mko baadhi ya wabunge mnaonekana vinara wa mvutano huo unaosababisha kuwagawa wabunge wa CCM katika makundi mawili na mnatajwa zaidi wawili.
Jibu. Ndiyo
Swali. Je ina maana katika chama chenu hakuna wengine na kwa nni msiwashawishi hao kuendeleza mapambano hayo.
SOURCE: Mwananchi.
Swali. Je ina maana katika chama chenu hakuna wengine na kwa nni msiwashawishi hao kuendeleza mapambano hayo.
SOURCE: Mwananchi.