Hali ya Mtwara mpaka sasa bado ni tete wananchi wa Magomeni wakimbilia hospitali ya mkoa

Unknown     10:16 AM    





 
Mwandishi wetu aliyepo Mtwara ametueleza kuwa hivi sasa baadhi ya wananchi wa eneo la Magomeni mkoani mtwara wamekimbilia katika Hospitali ya Mkoa wa Mtwara Lugula wakihofia usalama wao kutokana na vurugu za kuchomwa kwa nyumba zao pamoja na vibanda vya biashara zilizotokea leo asubuhi katika eneo hilo Mwanamke mwingine anayekadiriwa kuwa na miaka 25 mjamzito ameuawa kwa kupigwa risasi maiti ipo Ligula. Maduka maeneo ya Magomeni yamechomwa moto ikiwamo pia mali za Askari magereza . Mwanafunzi wa Chuno amefikishwa hospitali Ligula na majeraha ya risasi mguuni. Kwa sasa inaelezwa kuwa katika baadhi ya mitaa hali imetulia na ni idadi ndogo ya wananchi ndiyo inayoonekana wakitembea mitaani isipokua eneo la magomeni ambako mbomu yanaendelea kusikika huku huduma za kijamii katika mji huo zikiwa zimesimama zikiwemo usafiri, huduma za kibenki na shule

 
CHANZO: ITV TANZANIA

,

Recommended

Like Us

Company

Legal Stuff

FAQ's

Blogroll

Subscribe to Newsletter

We'll never share your Email address.
© 2015 Umbeya Specially. Blogger Templates Designed by Bloggertheme9. Powered by Blogger.