Na Imelda Mtema
DAAH! Pati ya kuzaliwa ‘bethidei’ ya mtoto wa Irene Pancras Uwoya na mumewe Hamad Ndikumana ‘Kataut’, Krrish imekuwa kama ya harusi, kwa namna ilivyofanyika, Risasi Jumamosi lina kila kitu.
Staa huyo wa filamu za Kibongo aliangusha bonge la sherehe kwenye Ukumbi wa Shekinah, Makonde, Mbezi Beach jijini Dar, Jumatano iliyopita na kuhudhuriwa na mastaa lukuki.
Krrish alikuwa akitimiza miaka miwili tangu alipozaliwa Mei 8, 2011 ambapo sherehe ilianza mchana hadi usiku mnene kukiwa na kila aina ya burudani hivyo kuwaacha watu midomo wazi kufuatia kufuru hiyo.
MAAKULI MWANZO MWISHO
Kwa mujibu wa ‘balozi’ wetu, wageni waalikwa walipoanza kuingia ndani ya ukumbi, walikuwa wakikaribishwa kwa vinywaji vya kila aina na chakula kilichotengenezwa kwa utaalam wa hali ya juu hata kabla pati hiyo haijaanza rasmi, zoezi ambalo liliendelea hadi mwisho.
WATOTO WATENGENEZEWA KAMA HOLLYWOOD
Katika shughuli hiyo, kulikuwa na michezo mbalimbali ya kisasa ya watoto walioalikwa ambao walijengewa vijumba ‘spesho’ vya kuchezea kama Hollywood, Marekani.
ULINZI MKALI
Ili kuhakikisha kuwa hakuna kitu kinachoweza kuleta ‘mizinguo’ na kuhatarisha burudani, kulikuwa na mabaunsa wapatao saba waliokuwa wameweka ulinzi mkali.
UWOYA, NDIKU
Huku watu wakiendelea kugonga ‘mpunga’, vinywaji na muziki, waliingia wazazi wa Krrish, Uwoya akifuatana na Ndiku wakiwa wamembeba mtoto wao na kusababisha shangwe za makofi na vigelegele.
MAPENZI MOTOMOTO
Uwoya na Ndiku, muda wote walionekana wakiwa katika mapenzi motomoto kwa kukimbizana ukumbini kwa mabusu ya kumwaga.
BONGO MOVIES
Katika mnuso huo, mastaa mbalimbali kutoka Bongo Movies walipoingia ukumbini walichangamsha sherehe kwani mara zote walikuwa wakifurahi na kuserebuka muziki.
JB AFUNGUA SHAMPENI
Kulikuwa na shampeni zipatazo arobaini ndani ya ukumbi huo lakini Steven Jacob ‘JB’ aliombwa kufungua moja kwa ajili ya kuziwakilisha nyingine huku watu wakimuimba; ‘Bonge la Bwana’ na kumfanya kuona soo kimtindo.
BIBI, BABU KRRISH
Chereko zilikolea baada ya baba na mama mzazi wa Uwoya, kujichanganya na wageni waalikwa huku wakicheza na kufurahi kwa pamoja.
WATOTO YATIMA
Ili kuonesha anajali watoto wengine ambao wazazi wao wametangulia mbele ya haki, staa huyo aliwaalika watoto yatima ili kusherekea na Krrish siku hiyo.
Hadi Risasi Jumamosi linaanua jamvi ukumbini hapo usiku, watu walikuwa wakiendelea kutandika ‘masanga’ na kuserebuka muziki.
source: GPL
Birthday ya mtoto wa UWOYA ni kama harusi!
Unknown
12:35 AM
Recommended
-
Anaitwa Gentriez Mwakitabu ni rapper wa River Camp Soldiers na mwanzilishi wa Chata ya Arusha Boy Na Arusha Girl. Logo hii ni moja ya se...
-
Hapa ni katika show ya Diamond huko Bukoba ,,nguo ya ndani tupa kule: Mwanamke akimwagiwa maji matakoni mbele ya watoto waliohudhu...
-
" Mimi ni mwanamke wa miaka 30 tatizo kubwa linalonitatiza ni kuwa wakati wa kufanya mapenzi na mr. Nitajuaje kama nami pia nimekojoa...
-
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Absalom Kibanda akiwapungia wanahabari wenzie mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Nd...
-
Inawezekana wengi wetu tukawa tunayatumia bila kujua kwamba tumekusidia kuyatumia. Haya ni maneno au kauli ambazo mume/mke anaweza mwambia ...
-
Kwa Mujibu wa Mtandao wa Kenyan Post Hizi ndio Picha za Msichana mmoja wapo ambae anakabiliwa na Mashtaka ya kukutwa wakifanya ma...
-
Socialite Huddah Monroe seems to be dogged by controversies in everything she lays her hands on. However, in a complete turn of events, th...
-
Inasemekana kuwa asilimia kubwa ya wanawake huwa hawafikii kabisa kilele kwa upungufu wa nyege au matatizo mengine ya kimaumbile tukiachili...
-
The star was photographed with légs spread while she was performing on stage.. We can't help but wonder what she was up to before the c...
-
Hivi karibuni mwanaume mmoja aliyefahamika kwa jina la Ezekiel Malika 'Baba Kulwa' amenaswa gesti na mkewe akiserebuka na shoga a...