Alichukiandika P-funk juu ya Profesa Jay kuchukua kadi ya chadema

Unknown     5:20 AM    

Jana ilikuwa ni siku nzuri kwa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) baada ya kumpokea mwanachama mpya Joseph Haule a.k.a Profesa Jay aliyekabidhiwa kadi ya Chama na mh. Joseph Mbilinyi a.k.a Sugu na John Mnyika.



Baada ya habari hizo kuenea wengi walianza kutabiri kuwa huenda mwaka 2015 Profesa Jay akagombea ubunge katika jimbo moja Tanzania.

P-Funk Majani yeye anaamini kabisa kuwa hilo linaweza kutokea na hatashangaa, kupitia akaunti yake ya Twitter jana (21 May) majani alimtumia ujumbe wa kumpongeza Prof. Jay na kumwambia kuwa hatoshangaa kama atakuwa mbunge kwa kutokana na kiwango chake cha kufikiri.

Hii ni tweet ya P-Funk Majani.

“Big up to @Profesa_Jay big things a gwan! Wudnt be surprised if u become an MP with ur level of thinking. #SALUTE King Kiboya for me!”

Profesa nae akamjibu:

“@P_Majani pamoja sana the super dupa producer Amini kuwa hatutakuangusha @jidejaydee IT’S ON NOW!!!!!!”


Recommended

Like Us

Company

Legal Stuff

FAQ's

Blogroll

Subscribe to Newsletter

We'll never share your Email address.
© 2015 Umbeya Specially. Blogger Templates Designed by Bloggertheme9. Powered by Blogger.